Pages

  • Latest News

    Friday, 4 July 2014

    ODAMA

    MTOTO mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ aliyesoma shule ya msingi mkoani Kigoma kisha kuhamia jijini Dar na kupitia kozi tofautitofauti kabla kutupa karata yake katika anga la filamu ndiyo tupo naye leo katika Exclusive Interview. 

    Mtoto mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ akiwa na marehemu Recho Haule enzi za uhai wake.
     Awali, hakuwahi kuwaza kama siku moja anaweza kuwa mwigizaji, lakini baadaye upepo ulibadilika na kujitengenezea jina la kazi, Odama. Kwenye makala haya amefunguka mambo mengi kuhusiana na safari yake ya uigizaji, twende pamoja:
     Mwandishi: Wasomaji wetu wangependa kujua historia yako kifupi?
    Odama: Nilianzia masomo yangu kule Kigoma baadaye nikahamia Shule ya Msingi Mburahati, sekondari nikamalizia Moshi mwaka 2000.

     Mwandishi: Nini kilifuata baada ya kumaliza masomo yako ya sekondari?
    Odama: Nilisoma kozi mbalimbali za kompyuta kisha ndipo nikajikuta nimekita nanga katika masuala ya filamu.

     Mwandishi: Ulianzaje na nani ambaye alikuunganisha na fani hiyo?
    Odama: Nilivutiwa na uigizaji ghafla, nikajiunga na Kikundi cha Kidedea, nikafanya mazoezi lakini bahati mbaya mmiliki wa kikundi hicho, Peace alifariki kikasambaratika hivyo nikawa nimepoteza uelekeo wa kisanaa.

     Mwandishi: Ulifanya nini baada ya kundi hilo kufa?
    Odama: Nilikaa kwa muda kisha baadaye nilikutana na ‘camera man’ mmoja anaitwa Musa Banzi ambaye alinikuta Holliday Inn, Posta nikiwa na rafiki yangu ndipo wakaniomba kushuti katika kipande cha wimbo wao baada ya mtu waliyekuwa wamempanga aje kuchelewa, baada ya kumudu uhusika vizuri katika video hiyo, kila mtu aliyekuwepo hotelini hapo aliguswa na mimi. Wakanishauri nijikite katika uigizaji.







    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ODAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top