Pages

  • Latest News

    Tuesday, 11 March 2014

    LOWASSA AKANA KUHUSIKA NA NOTI

    Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa, amekanusha kuhusika na noti zenye thamani ya shilingi 500/= ambazo zinaonyesha sura yake sehemu inapokuwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

    Noti hizo ambazo zimesambazwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii kwa muda upnaokaribia wiki moja sasa, zinafanana na noti za shilingi mia tano za sasa isipokuwa hizi zina sura ya Lowassa.
    Akikanusha kuhusika kwake na noti hizo, Lowassa alisema “kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumhusisha na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.”

    “Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha yangu. Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi,” amesema Lowassa.

    Aidha, Lowassa amesema “naheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini ni muhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.”



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LOWASSA AKANA KUHUSIKA NA NOTI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top