MTOTO wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa anayeitwa Frederick
Lowassa anachunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa
Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania.
Fedha hizo zinahusishwa na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya paundi
za Uingereza 475,000 (takriban Shilingi bilioni moja) katikati ya
Jiji la London. Nyumba hiyo ipo mtaa wa Leinster Gardens, jijini
London.
Hata hivyo, hakuna ofisa yeyote wa Serikali ya Tanzania aliyekuwa
tayari kuzungumzia suala hilo, pamoja na kuwapo taarifa kwamba tayari
vyombo vya dola vya Tanzania vimekwisha kuhusishwa katika uchunguzi
huo.
Maofisa wa Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) wanaohusika na
uchunguzi wa fedha haramu, pamoja na Mkurugenzi wa upelelezi wa
Makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba, wamekwepa kuzungumzia suala
hilo.
Source: Raia Mwema, Toleo la 161
HIVI WATANZANIA TUMELOGWA???
KWA NINI TUNAPENDA KUSHABIKIA MAOVU??
LOWASSA HAFAI KABISA KUWA HATA BALOZI WA NYUMBA KUMI
0 comments:
Post a Comment