Dar
es salaam. Waziri
wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasubiri kukamilika kwa utaratibu
wa CCM wa kugombea urais ili aingie rasmi kwenye mbio hizo kwa kuwa
anaridhika na mambo matatu ambayo anasema yanamfanya ashawishike
kugombea nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini.
Sitta,
mwanasiasa mkongwe na Spika wa Bunge la Tisa, ni mmoja kati ya makada
wa chama hicho tawala wanaotarajiwa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya
CCM kugombea urais kumrithi Jakaya Kikwete, ambaye anamaliza vipindi
vyake viwili vya urais Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Sitta alisema zaidi ya mambo hayo
matatu, anaamini ana ushawishi mkubwa na Watanzania wengi wanamwamini
katika utendaji kazi wake.
“Nina
mengi nimefanya kutokana na historia yangu ya kiutendaji na ndiyo
nitakayoitumia kama mtaji utakaonibeba kwenye harakati hizi,”
alisema.
Sitta,
ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, alitaja mambo hayo
matatu ambayo ni mtaji wake kuwa ni uendeshaji wake wa chombo hicho
cha kuandika Katiba, uendeshaji wake wa Bunge na uzoefu wake wa muda
mrefu kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kushika.
Sitta,
ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, alitaja mambo hayo
matatu ambayo ni mtaji wake kuwa ni uendeshaji wake wa chombo hicho
cha kuandika Katiba, uendeshaji wake wa Bunge na uzoefu wake wa muda
mrefu kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kushika.
“Niliendesha
Bunge la Katiba kwa mafanikio na hata kupatikana kwa Katiba
Inayopendekezwa,” alisema Sitta.
“Watanzania
wataangalia wenyewe historia yangu kwani mimi ndiye mwenyekiti
niliyefanikisha kutimiza ndoto za Watanzania kupata Katiba mpya
kupitia Bunge Maalumu la Katiba, haikuwa rahisi katika tukio hilo,”
alisema.
Hata
hivyo, Bunge la Katiba halikuisha kwa maridhiano baada ya wajumbe
kutoka vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kususia
vikao kwa madai kuwa chombo hicho kiliweka pembeni Rasimu ya Katiba
iliyokuwa na maoni ya wananchi.
Juhudi
za Sitta kuwarejesha vikaoni ziligonga mwamba, lakini mchakato
ukaendelea hadi Katiba Inayopendekezwa ilipopatikana.
Sitta
alisema mtaji wake mwingine katika mbio za urais ni na kuimarisha
demokrasia ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
“Mimi
ndiye niliyebadilisha Bunge baada ya kubadilisha kanuni za Bunge
mwaka 2007, ambazo zilitoa uhuru, haki na usawa kwa wabunge wote bila
kujali wapinzani,” alijigamba.

0 comments:
Post a Comment