Dar
es Salaam. Majambazi
wamemuua kwa risasi Sista wa Kanisa Katoliki Clencensia Kapuli (50)
na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijajulikana.
Pia,
katika tukio hilo lililotokea jana saa nane mchana eneo la Riverside,
Ubungo, Dar es Salaam, dereva aliyekuwa akimwendesha Sista Kapuli,
Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.
Sista
Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mwenyeheri
Anwarite, Makoka Jijini Dar es Salaam alikuwa mhasibu wa parokia hiyo
ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha
Ufundi Stadi Makoka.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliyefika katika Kituo
cha Polisi Urafiki kufuatilia tukio hilo alisema Sista Kapuli na
sista mwenzake wakiwa katika gari aina ya Toyota Hilux, walikuwa
wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha na
walipita Riverside ndipo walipopatwa na mkasa huo.
“Bado
hatujajua ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa kwa kuwa Sista Kapuli
ndiye alikuwa mhasibu na ndiye aliyekwenda kuchukua fedha hizo,
subirini tutakapokwenda benki kuuliza ni kiasi gani cha fedha
alichukua na tutawajuza,” alisema Wambura.
Kamanda
huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili ukisubiri taratibu za mazishi.
Shuhuda
wa tukio hilo, Gadi Kinyamagolo alisema masista hao walikwenda
Riverside kununua mchele katika moja ya maduka ya jumla.
“Mara
baada ya kumaliza kununua mchele kama kilo 10 hivi walipanda katika
gari wakiwa wawili na kabla ya kuondoka zilifika pikipiki mbili
zikiwa na watu wanne, zikasimamisha gari hilo huku mmoja akiwa
amevalia kininja na mwingine aliyevaa kawaida, wote wakiwa na silaha.
Wengine wawili walibaki kwenye pikipiki.
“Kisha
nikaona wanapasua kioo cha nyuma ambapo kulikuwa na sista mmoja na
mwingine alikuwa mbele, wote wakiwa na mikoba ambayo majambazi hao
waliiomba,” alisema Kinyamagoro na kuongeza:
“Walianza
kuwaambia tupe mikoba huku majambazi hao mmoja akiwa amesimama upande
wa dereva na mwingine upande wa pili wa gari alipokuwa sista
aliyeuawa lakini masista wale hawakutoa mikoba hiyo.”
Kinyamagoro
alisema: “Baada ya mabishano, sista aliyekuwa nyuma alifungua
mlango na kukimbilia katika duka walilonunua mchele na yule aliyekuwa
mbele alipofungua mlango akitaka kukimbia alipigwa risasi shingoni na
kutokea upande wa pili na kuanguka nje ya gari.
“Baada
ya tukio hilo majambazi hayo yalichukua mikoba miwili na kuondoka
nayo. Kwa kuwa mimi nilikuwa karibu nililala chini na eneo hili
lilikuwa kimya, watu walikimbia na wengine tulilala tukaacha wafanye
kazi yao

0 comments:
Post a Comment